Tarehe 20 mwezi huu pale New Maisha Club jijini Dar es Salaam, rapper Cyrill Fransisco aka
Kamikaze na CEO wa Wakacha Ent atazindua documentary yake inayozungumzia maisha yake
ya muziki mpaka alipo sasa.
Leotainment imekaa na rapper huyo kutoka Singida kutaka kujua zaidi kuhusiana na
Documentary hiyo.
Leotainment: Nini kimekusukuma uandae
documentary yako mwenyewe?
Cyrill: Kikubwa kilicho ni inspire ni mimi kufika hapa nilipo nikimaanisha kimuziki. So najua mashabiki wangependa sana kujua nilivyoanza,
ilikuaje, maana wamezoea kusikia story tu mtu akielezea kwenye nyimbo. Sasa this time around watapata kuiona live jinsi ilivyokua. Basically ni inspiration ambayo imetokana na mashabiki na mimi pia.
Leotainment: Kwanini umeiita FROM DAY ONE?
Cyrill: Nimeiita FROM DAY ONE simply
because inaelezea kila kitu nilivyo anza kwenye muziki toka siku ya kwanza mpaka kufika leo hapa nilipo na pia napoelekea.
Leotainment: Akina nani wanaonekana humo? Washkaji tu ama wazazi pia wanaonekana?
Cyrill: Watakuwepo watu wengi kidogo
wakielezea ni nini kiliwasukuma mpaka wao kunisaidia mimi,akiwemo mama yangu mzazi,A.Y,uncle zangu, B12 pamoja nawatu wengi tu ambao walisaidia kwa kiasi kikubwa
mimi kufika hapa..ndugu watakuwepo pia.
Leotainment: Ina matukio tangu utotoni pia? Mambo kama yapi?
Cyrill: Matukio ya utotoni yapo pia mfano nilivyoiba hela ya mama kabatini kununua CD ya Snoop Dogg ,nilivyotoroka shule kwenda
kurecord studio mwishowe nikalala huko bila kurecord na vitu vingi tu.
Leotainment: Nani ameproduce documentary na itakuwa na muda gani? yaani running time.
Cyrill: Kuna Yudii, jamaa mmoja video director anaitwa Yusuf, Lamar na pia Qwisar kwenye graphics. Documentary itakuwa ya saa moja na dakika ishirini hivi.
Leotainment: Baada ya uzinduzi utaiuza ama?
Cyrill: Hapana haitauzwa, itatolewa bure tu! Hii ni kama zawadi ya mashabiki wangu walionipandisha mimi kuwa hapa na bado kunipa support mpaka leo.
Leotainment: Kingine cha ziada ambacho
ungependa watu wajue kwenye uzinduzi huo?
Cyrill: Ni kwamba itaonesha baadhi ya show zangu,pia jinsi nilivyo record baadhi ya nyimbo. Pia wataona jinsi mimi na Prezzo tulivyokua
tuna record. Pia watapata nafasi kusikia
akizungumzia project yetu.
Nolniz Blog inamtakia Cyrill kila lakheri kwenye uzinduzi wa FROM DAY ONE!
©2012 Nolniz Blog™
No comments: