728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
01 June 2012

PNC kurudi tena | Sasa akiwa member ndani ya kundi la MTANASHATI

MSANII maarufu wa Muziki wa Kizazi Kipya Pancras Ndaki maarufu kwa jina la 'PNC' amejiunga rasmi na kundi la Mtanashati ambalo ofisi zake ziko Magomeni jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia hilo PNC alisema kuwa mkataba aliongia na kundi hilo ni wa kudumu na ameahidi kufanya kweli ndani ya kundi hilo ambalo linakuja juu katika Muziki wa Kizazi Kipya.

Msanii huyo ambaye sio mgeni katika game na mwenye sauti ya kipekee ameahidi kuwa watu watarajie mengi na makubwa kutoka kwake. Aliongeza kuwa, kwa sasa ametoa ngoma yake mpya inayoitwa binadamu ambayo sasa iko hewani tangu Mei 30 mwaka huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa kundi la Mtanashati, Ustaadh Juma Namsoma amemteua PNC kuwa meneja wa kundi hilo na kumuahidi masalahi mazuri kwa kuwa ana imani kubwa na msanii huyo.

All tha Best Mtanashati kwani tunauhakika mmejifunza kutoka kwa makundi mengi yaliyokuwepo na kuvunjika na hatutarajii hivyo kwenu


©2012 Nolniz Blog™
PNC kurudi tena | Sasa akiwa member ndani ya kundi la MTANASHATI Reviewed by Nolniz on Friday, June 01, 2012 Rating: 5 MSANII maarufu wa Muziki wa Kizazi Kipya Pancras Ndaki maarufu kwa jina la 'PNC' amejiunga rasmi na kundi la Mtanashati ambalo ofisi...

[][carousel1]

No comments: