728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
18 July 2012

Kuzama kwa Mv Seagull ni Mwezi mmoja tuu baada ya kuzima majini

Wakati watanzania wakiwa hawajapona majeraha ya kuwapoteza ndugu zao katika ajali ya Meli ya Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana, Meli nyingine ijulikanayo kama Mv Seagull imezama majini ikiwa safarini ikitokea Dar es Salaam kuelekea Visiwani Zanzibar.
Meli hiyo ambayo kwa mujibu wa taarifa za mwanzo  ilikuwa na abiria wapatao 200 imezama na mpaka wakati huu  harakati za uokoaji zinaendelea na watu wakiendelea kuokolewa huku wengine wakielea juu ya maji kwa msaada wa maboya. Ingawa taarifa za vifo hazijatolewa bado ila ukweli kwamba vifo vipo.
Tukija kuiangalia historia ya hivi karibuni ya Meli hii iliyozama Leo tunajionea mwenendo wake mbaya kwani imesharipotiwa matatizo mengi kadha wa kadha lakini ndo hii imeendelea mpaka kupelekea hili la leo.
Mapema mwezi wa tano (12/05/2012) GAZETI LA MWANANCHI liliripoti kuzima moto kwa  Meli hii ikitokea Pemba kuelekea Unguja katikati ya maji na kusababisha tafrani kubwa kutoka kwa wasafiri waliokuwamo ndani ya meli hiyo na iliwalazimu kubakia melini mpaka ukarabati ulipomalizika ndipo safari ikaendelea.
Vipi baada ya tukio/ matukio ya mwanzo, hatua gani zilichukuliwa katika kuhakikisha usalama wa wasafiri unaongezeka na kupunguza matukio kama haya???
Tunawaombea wote waliokutwa na mkasa huu na Habari zaidi juu ya ajali hii tutaendelea kukujuza...

©2012 Nolniz Blog™
Kuzama kwa Mv Seagull ni Mwezi mmoja tuu baada ya kuzima majini Reviewed by Nolniz on Wednesday, July 18, 2012 Rating: 5 Wakati watanzania wakiwa hawajapona majeraha ya kuwapoteza ndugu zao katika ajali ya Meli ya Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana, ...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: