728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
03 July 2012

RAP RACE 2012 | HARAKATI ZA KUINUA VIPAJI VYA MUSIC TANZANIA




Katika kuendeleza na kuhakikisha Muziki wa Hip Hop Tanzania unakua na wanapatikana wanamuziki wenye vipaji vya uhakika, mwishoni mwa wiki hii mjini Arusha shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama RAP RACE lilifikia tamati yake na wakapatikana miamba wa mashahiri na kutunukiwa zawadi zao!

Ili kujua mengi na nini kilifanyika Nolniz Blog ilipata nafasi ya kufanya mahojiano na mdau mkubwa katika kuiwezesha event hiyo,John Blass maarufu kama John B moja ya majaji na pia Producer ndani ya Grand Master Records alikuwa na haya aliyoweza kushare nasi:
John B


               NINI HASA LENGO NA MADHUMUNI YA RAP RACE?
"Lengo kuu la Rap Race ni kuinua vipaji na zaidi ni kusaidia vijana ambao hawawezi ingia studio, Zaidi ya kupata video na Audio kuendeleza kujenga kipaji chao kwa mafunzo zaidi, washiriki walikua wanajiandikisha kwa kuchangia kiasi cha Sh5000 za Kitanzania"


VIGEZO GANI VILIVYOZINGATIWA KUWAPATA WASHIRIKI NA HATIMAYE MSHINDI?
"Kabla ya kuingia tulipokea washiriki wote waliojitokeza.. Hii ndiyo ilokuwa sababu kuu ya kufanya usaili wiki mbili zilizopita kuhakikisha tunapata wachache ambao tulikua nao juzi kwenye fainali, kuhusu vigezo, ni vingi kuanzia kiwango msanii alichoendelea kwa muda wa maandalizi, umiliki wa jukwaa, utoaji sauti, utayari, uzingatiaji wa misingi, kushika mic na pia ubunifu...."


                   UDHAMINI WA ISUE YENYEWE!!
"Mwanzoni zilikuwa harakati binafsi ila tukaona kuifanya bora zaidi ni vizuri kushirikiana na Kampuni nyingine kweli wametudaisia sana.... Na ninatoa shukrani kwa wadhamini wetu Sosh Graphix, Radio 5, Sibuka Tv, Sibuka Fm, Triple A Fm, Club AQ, MNP investments na Helpinf Hands pamoja na Team nzima ya Grandmaster Production"



MAONI NA UJUMBE WA JOHN B KWA FANS NA WASHIRIKI KWA UJUMLA;
"...Zaidi ni shukrani kwa fans wote waliojitokeza ku show love... Ilipendeza sana... Vijana wanahitaji support kubwa kama ile, kwa Producers waliokuwepo Daz Naledge na Mosco na uongozi wa Kazawaza... Tuzidi kuwa pamoja na kwa mwendo huo naamini tutafanya mengi na tutafika mbali. Heshima pia kwa mwenye Blogs na websites kwa kutubeba maana zote hizi ni harakati na bila wote kuvutia mwelekeo mmoja tusingefanikisha" Alimalizia John B
Goodluck "Mshindi no.1 RAP RACE 2012"
RAP RACE 2012 | HARAKATI ZA KUINUA VIPAJI VYA MUSIC TANZANIA Reviewed by Nolniz on Tuesday, July 03, 2012 Rating: 5 Katika kuendeleza na kuhakikisha Muziki wa Hip Hop Tanzania unakua na wanapatikana wanamuziki wenye vipaji vya uhakika, mwishoni mwa wiki...

Labels:

[Video][carousel1]

No comments: