728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
15 July 2012

Ukweli Kuhusu vurugu zilizotokea Ndago Singida

"Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMA iliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese.
Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa
wamelewa chakari. Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi mawe yapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.
Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na
kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma
ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba. Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi.
Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.
Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.
Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara
ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa
Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na
kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa
wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha
Ualimu cha Kinampanda.
Taarifa nilizozipata baadaye ni kwamba yule
kijana aliuawa ndani ya nyumba ya mtu kando kidogo na mkutano ulipokuwa unafanyika. Mtu huyo pia anatajwa kuwa kada wa CCM aliyekuwa anagombea ukatibu kata na ndiye aliyepewa fedha na Mwigulu kuratibu shughuli nzima ya fujo.
Sina uhakika kama mikutano ya leo ya CHADEMA itafanyika kwa sababu vijana wameshaanza kukamatwa na kuna hatari polisi wakazuia mikutano ya leo.
Pamoja na yote haya, Mwigulu watu
wanamchukia sasa hivi kwa mambo ya kihuni
anayoyafanya. Hatujuwahi kuwa na Mbunge wa namna hii katika Jimbo hili".

Chanzo cha Habari hii na maelezo haya ni kwa mujibu wa aliyejitambulisha kama
Mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, Singida na ni katika kujuzana

nimekujuza ila wewe ndo unayejua utakavyoichukulia

Ukweli Kuhusu vurugu zilizotokea Ndago Singida Reviewed by Nolniz on Sunday, July 15, 2012 Rating: 5 "Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya...

[Breaking News][carousel1]

No comments: