728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
12 August 2012

Ay ft Sean Kingston Project kutoka mwezi ujao

Msanii anayeonesha mafanikio makubwa na mkongwe ndani ya wa Music wa kizazi kipya nchini Tanzania, Ambwene Yessaya maarufu kama AY yupo katika hatua za mwisho za kumalizia kazi yake na Kichwa kingine Sean Kingston kutoka Jamaica ila aliyehamishia majeshi yake ndani ya U.S.A. Pamoja na kalenda nyingi alizokuwa akipigwa  kutokana na Kingston kuwa katika ziara yake ndefu ya kimuziki, ila kutokata tamaa kwake Ay pamoja na uvumulivu wake hivi karibuni matunda yake yanatarajia kuonekana kwani kwa sasa anajipanga kuibuka ndani ya Los Angles Marekani kwa ajili ya kazi hiyo.
Ay alipata ofa ya kufanya kazi na Sean Kingston bure ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipowasili Tanzania mwaka juzi kutokana na kukubali kile ambacho Ay anakifanya. Kufanya kazi na msanii mkubwa kama Kingston stio kitu kidogo kwani Jose Chameleone kutoka Uganda naye amepewa ofa hiyo ila yeye ameambiwa atailipia US $30,000 ikiwa ni zaidi ya milioni (45).
Katika project hiyo Ay amesema ameshafanya kazi mbili ambayo moja ilishakamilika japo hajaiachia bado ila kwa sasa anaenda kufanya hiyo ya pili ikiwa ni pamoja na Video..!! Kazi hii ya pili aliipata ikiwa ni baada ya Kingston kuiona Video ya PARTY ZONE na kuikubali kuona kijana anafanya kweli...!!

Hatua hizi zikiendelewa kufatwa na Artists wengine Tz mafanikio ya kazi zao ikiwa ni pamoja na kujulikana zaidi kidunia na kuutambulisha mziki wetu vitafanikiwa

Soma alichokiandika Millard Ayo   

©2012 Nolniz Blog™
Ay ft Sean Kingston Project kutoka mwezi ujao Reviewed by Nolniz on Sunday, August 12, 2012 Rating: 5 Msanii anayeonesha mafanikio makubwa na mkongwe ndani ya wa Music wa kizazi kipya nchini Tanzania, Ambwene Yessaya maarufu kama AY yupo kati...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: