Fans wote wa mziki mzuri kutoka Arusha, jina Jambo Squad sio geni kwao maana ni moja kati ya kundi linalofanya mziki wa aina yake unaowashika watu wengi wa rika na jinsia zote!! Huku wakiwa na track kibao kama Mamong'oo, 'Disko malapa', 'Tofauti sana na story' waliomshirikisha G-Nako, Temana na mimi, na nyingine kibao. Kama kawaida yao kila siku wanaendelea kufanya vipya na vikali na kila inapotoka mpya inakuwa ni hatari zaidi ya iliyotangulia na kwa wakati huu wataachia Jointi mpya linalokwenda kwa jina la 'Mpori Mpori' ikiwa ni bonge moja la story, boonge moja la Idea. Jambo Squad wanawataka fans wao na wote wanaopenda mziki mzuri kukaa tayari kwa ngoma yao hiyo na kama kawaida yetu Ikishakuwa official release wataisababisha kitaa hichi cha nolniz.blogspot.com!! Stay Tune, Usikose kuwa wa kwanza katika hii
©2012 Nolniz Blog™
No comments: