Zaidi ya waandishi wa habari 240 kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha A.J.T.C wameanza mafunzo ya ujasiria mali ikiwa ni kama moja ya nyenzo ama njia ya kuwajengea mazingira ya kutambua fursa walizonazo.
|
Mkuu wa Mafunzo AJTC Bw.Joseph Kagiye Mayagila |
Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa Chuo hicho Bw.Joseph Kagiye Mayagila amesema, umaskini wa Watanzania ni wakujitakia hivyo kwa mtu anayetaka kuwa tajiri akiamua anaweza...
"Mmea pekee ndio unaweza ukawa na kisingizio cha kutopata mahitaji kwa wakati unaotaka mpaka uamuliwe na watu ama mtu kwa kuwa hauna mdomo wa kusema kuwa nini unataka... Wenzangu na ninyi hapa mna maamuzi, aidha muamue kuwa maskini ama matajiri kwani mnauwezo wa kufanya kulingana na jinsi mnavyotaka kwani umaskini sio kilema" alisisitiza.
Katika kumalizia Bw.Joseph Mayagila Alimalizia akisema huu sio wakati wa kuishi kwa kuiga bali kila mmoja wetu ana wajibu wa kufanya kazi kwa maslahi yake na nchi kwa ujumla,na kuwataka waandishi hao kutokata tamaa ya maisha.
|
Madam Neema & Veridiana Wakiwa katika usikivu kufuatilia semina ya ujasiriamali |
Semina hiyo imeanza leo na baadhi ya wakufunzi wamewasilisha mada zao kuhimiza ujasiriamali na kusisitiza kila mtu kudhamini kazi anayoifanya hususani biashara walizoanzisha ama watakazo zianzisha
|
Madam Leah & Mr Modaha katika semina |
Mwisho
©2012 Nolniz Blog™
No comments: