Grandmasters Records iliyopo mjini Arusha Chini ya John B, John Blass baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu sasa imerudi tena online katika kufanya vingi na vikubwa katika Music Production.
Akiongea na Nolniz Blog Producer na mmiliki wa studio hizo, Jan B amesema kwa sasa yupo Arusha kwa ajili ya kazi nyingi za music katika level nyingine kabisa.
Kwa kuanzia, Grandmasters Records Arusha wameanza na ngoma iliyopewa jina 'WAZI' ambayo mtu mzima Cannibal ataiwakilisha Kenya. Kutoka Tanzania atakuwepo mzee mzima JCB, MO Plus, Nakaaya, Nikki wa Pili, Bonta, Joes, Slim Dizzy na Gnako (A city Finest)
Katika kuongeza ladha zaidi haikuishia hapo kwani yupo pia msanii mwingine kutoka Zimbabwe Thai Tha na Tricky D.T kutoka jiji la Madiba, South Africa.
"Nataka watu wajue Grandmasters is Back Online.. Na mimi nipo.... Mengi sana yanakuja na fans pia wategemee mengi ambayo bado hayajawahi kufanyika" Alimalizia Jan B
Baadhi ya ngoma ambazo zimefanyika ndani ya Studio za Grand ni kama..
1- Nikikupata/ Nieleze - John Woka ft Keisha,
2- Wakusindikiza,
3- Sio kwa ajili yaa (Nembo mbaya) wa Bou Nako ft G Nako,
4- Press Play North Dwellers ft Josline, Nakaaya & Tippi.
5- Ngastuka,
6- Disko malapa na nyingine kibao ni kati ya nyimbo zilizofanywa ndani ya Grand Masters Records.
People stay tune, vingi vizuri kutoka Grand Masters Records vinakujia..... kama kawaida vitasomeka humu humu pia.
©2012 Nolniz Blog™
No comments: