728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
04 September 2012

Katika kutafuta umaarufu Producer ajibatiza umeneja wa kundi kusaka sifa

Katika hali isiyo ya kawaida na ya kushangaza, jamaa mmoja mjini Arusha kupitia media ameamua kujivisha umeneja wa kundi la Mecca Cheka lenye makazi yake mjini Arusha na kutangaza kwamba vijana hao wapo chini yake na kazi zao zote anazisimamia yeye kitu ambacho sio kweli.
Kutokana na jambo hilo kuwa na sitojua nyingi vichwani kwa watu ikiwa ni kutokana na wengi kutoelewa nani mkweli kati yao, Nolniz Blog iliamua kuwatafuta Meccacheka kujua ukweli wa jambo hili kwao likoje na Joseph kwao ni nani.

 Katika mahojiano na mmoja wa member wa kundi, Almando Mwirora alikiri kunamtu anajyejitafutia ujiko kupitia wao (MeccaCheka) na kwamba ni kweli kuna mtu amesema kwamba yeye ni meneja wa MeccaCheka lakini wao wanamtambua mtu huyo (Joseph Tairo) kama producer tuu na wanashangazwa ni vipi ajiite Meneja wakati hata u producer wenyewe anaufanyia studio isiyoeleweka na ameamua kutumia njia hiyo kwa nini wakati hawajawahi kuongea naye kitu kama hicho na kwamba wao hawapo chini ya management ya mtu yeyote mpaka muda huu

"Jamaa unajua anatuchafulia tuu na simuelewi kwa nini... watu wengi wanatamani kuiendesha MeccaCheka lakini inakuwa ngumu kwao maana yeye (Joseph) amekuwa kikwazo kwetu na ameamua kujitangaza kama meneja wetu wakati sisi hicho kitu hatujui kakitolea wapi kwani zaidi ya New Way Studio's anayoimiliki hatumtambui kwa chochote kile...!! Jamaa katukera sana na hata kazi naye sidhani kama tutaweza kufanya kwa ambayo ameyafanya ila tunapenda fans wetu na wadau wote kwa ujumla watambue kwamba MeccaCheka haimtambui huyo Joseph na kwamba hatuna management yoyote inayotutawala...."

Sasa wasanii wenyewe kumbe hawamtambui mtu huyo na bado yeye anajiita meneja, Vipi kujisifia kuna maana gani wakati bado unakuwa kama unawaharibia wenzako.....??

 ©2012 Nolniz Blog™
Katika kutafuta umaarufu Producer ajibatiza umeneja wa kundi kusaka sifa Reviewed by Nolniz on Tuesday, September 04, 2012 Rating: 5 Katika hali isiyo ya kawaida na ya kushangaza, jamaa mmoja mjini Arusha kupitia media ameamua kujivisha umeneja wa kundi la Mecca Cheka leny...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: