Record Label ya Wanene Entertainment yenye makao yake makuu mjini Arusha iliyopo chini ya C.E.O Darsh Pandit, imeendelea kuongeza wasanii wapya ndani ya label hiyo kutoka pande tofauti tofauti za Dunia. Katika muendelezo huo wa kuingia mikataba na wasanii mbali mbali wanaofanya mziki katika level za kimataifa, awamu hii wamemtambulisha Louis Hammock kutoka Uingereza ndani ya Label hiyo.
Louis Hammock ambaye sasa naye ataitwa Mnene na kama kupiga hodi ndani ya Tanzania na fans wote wa mziki mzuri ameachia kazi yake ya kwanza ambayo ni Mixtape iliyobatizwa jina la "Untitled"
Hammock amekua msanii wa pili kutoka nje ya Africa kujiunga na Wanene Entertainment akiwa ametanguliwa na The Artist msanii kutoka Marekani. Mbali na The Artist, yupo raia mwingine waweza muita Arusha Boy, Gentriez Mwakitabu lakini yeye ndiye anaye iwakilisha Tanzania kama msanii ndani ya Wanene Ent
Katika harakati hizi za kuupaisha mziki wetu kutoka Tanzania ili dunia nzima ielewe tunachokifanya kama watanzania, Nolniz Blog inampa shavu Darsh (C.E.O wa Wanene) kwa harakati hizo ambazo sasa zinaonekana za kuendeleza Game ya Music wa Tanzania World Wide
Kupitia Facebook waweza mpata kama Louis Hammock
Na katika Tumblr kwa kubonyeza hapa Louis Hammock
Waweza download mixtape ya Louis Hammock "Untitled" hapo chini
©2012 Nolniz Blog™
No comments: