Huyu ni mwanamuziki chipukizi kutokea Moshi akiwa anaitwa Maua Sama. Ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Ushirika na Biashara Moshi [MUCCOBS], kwa mara ya kwanza anasikika katika wimbo wake ambao amemshirikisha MwanaFA, ikiwa ni wimbo unaomtambulisha katika ulimwengu wa muziki wa kizazi kipya.
Kwa sasa Maua anafanya kazi chini ya uangalizi wa LifeLine/ T.I.A Inc. label ya muziki ambayo inasimamia kazi za muziki za MwanaFA.
''So Crazy'' ni ngoma iliyofanywa na Producer Marco Chali wa MJ Records.
Kuwa wa kwanza kuisikiliza track hiyo hapa chini...
No comments: